Na MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa CCM Tanga, Rajab Abdallah amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maendeleo makubwa Tanga na kuondoa changamoto mbalimbali Mkoani humo ikiwemo suala la elimu kwa kuendeleza shule za kata.
Aliyasema hayo jana Wilaya ya Muhenza wakati akitoa salamu za Chama Mkoa huo, katika ziara ya Rais Dk.Samia mkoani humo,
Alisema katika suala la elimu Rais Dk.Samia ameendelea kuchochea elimu kwa Watanzania kupitia sekondari za kata, zinazowezesha kupatikana wataalamu mbalimbali watakao saidia Taifa.
Katika hatua nyingine alisisistiza kuwa, watahakikisha Mkoa wa Tanga unakua wa kwanza, kuongoza kwa kura za Urais katika Uchaguzi Mkuu.