The Dipromats yatangaza timu ya kutoa huduma katika mikutano, harusi na sherehe mbambali za kisasa
Kampuni ya The Diplomats imezindua rasmi utoaji huduma zake kupitia matukio ya mikutano ya kiserikali na binafsi, vikao vya harusi, sherehe za harusi, zinazotekelezwa na vijana maalumu wenye taaluma ya itifaki waliobobea katika diplomasia.
Akielezea utoaji wa huduma hizo leo, Meneja wa Kampuni hiyo, Antony, alisema lengo la kampuni hiyo kuanzia utoaji wa huduma hizo ni kuwahudumia Watanzania katika matukio mbalimbali kwa utaratibu mzuri unaokubalika kitaifa na kimataifa.
"Mbali na huduma hizo, kampuni yetu itakuwa na huduma zingine za walinzi binafsi, (Body guard), catering, mc, music na huduma zingine kama hizo.
"Tumeamua kufanya hivi kutokana na uhitaji mkubwa uliopo katika soko, kwani changamoto ni kubwa katika matukio mbalimbali yanayofanyika kupitia mikutano, hakuna wahudumu wazuri waliopata mafunzo ya itifaki ya mapokezi ya wageni kwa kufuata utaratibu na heshima ya mtu, hivyo tunao wataalamu wabobezi, waliosomea na wenye nidhamu kubwa," alisema.
Naye, Mdau wa Kampuni hiyo, Mc, Antony Luvanda alisema alisema zamira hiyo inatokana na kazi njema iliyofanywa na serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kufungua Taifa katika nyanja ya diplomasia hivyo kuchochea kufanyikaji wa mikutano ya kimataifa.
Alisema wamejipanga vyema kuhakikisha wanatoa huduma njema kwa Watanzania, kupitia uandaaji mzuri wa matukio ya mikutano hiyo kwa mpangilo mzuri na kufuata itifaki.
The Dipromats yatangaza timu ya kutoa huduma katika mikutano, harusi na sherehe mbambali za kisasa
Reviewed by Gude Media
on
March 01, 2025
Rating:
