Na MWANDISHI WETU
Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya kibiti, Juma Kasssim Ndaruke ametoa rai kwa wa Umoja wa wanawake (UWT Kibiti) kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumtafutia kura za Urais kila eneo la Wilaya Kibiti.
Ndaruke ametoa rai hiyo leo, wilayani humo, katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, huku akisisitiza Wanawake kutafuta kura za kutosha kwa Rais Dk.Samia.
Amesema Wanawake wana deni kubwa kwa Rais Dk.Samia mwaka 2025, kwa kuhakikisha wanafanya jitihada za kutosha za kutafuta kura za urais kila pembe ya mtaa ya wilaya Kibiti kwani mgombea wa Urais ametokana na UWT.
"Tusije kucheza na mtu yoyote mwenye virishia vya kutaka kupunguza kura za CCM, maeneo yote, niwaombe sana tusidhubutu kucheza na kudharau mipango yoyote itakayoleta viashiria vya kupunguza kura Dk.Samia maeneo tunayongoza, tukiruhusu mipango, tutakuwa tumehudumu ,twende kwa nguvu kubwa kuhakikisha wilaya ya kibiti inakwenda wilaya kwanza kutafuta kura za mgombea wa urais 2025." amesema Ndaruke.
Ameongeza kuwa, katika kipindi cha uchaguzi wapo wamama wamepanga kugombea na wengine kutetea nafasi zao isije ikawa vita kwa wanaotetea nafasi zao, wale waliojiandaa kugombea na kutete nafasi zao wakatetea kwa nguvu zote.
Aidha Ndaruke amesema nafasi hizo ni mali ya chama cha mapinduzi haina haja ya wanachama kugombana kwenye kugombea nafasi hizo huku asisitiza kuheshimu kanuni na taratibu za chama cha mapinduzi.