DC Mpogolo atunukiwa tuzo
Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net) Wilaya ya Ilala umemtunuku tuzo maalumu Mkuu wa wilaya hiyo Edward Mopogolo ya kutambua mchango wake katika kujenga jamii salama,jumuishi na yenye usawa wa kijinsia
Mpogolo amekabidhiwa tuzo hiyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo.
Ameushukuru mtandao TPF Net kwa kutambua mchango huo na kwamba tuzo hiyo ni heshima kubwa kwake na wananchi wa Wilaya ya Ilala.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na SSP Latifah Chicco (RFBO Ilala), ASP Sophia Dilunga (OCS Kati na A/Inspekta Husna wa Ofisi ya RFBO Ilala.
DC Mpogolo atunukiwa tuzo
Reviewed by Gude Media
on
August 06, 2025
Rating:
