RC Chacha aamuru viongozi wa AMCO 32 wakamatwe
IGUNGA TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ameamuru viongozi vya AMCO 32 wakamatwe kwa kudaiwa kuchezea mizani ya kupimia pamba na kuwaibia wakulima wilayani Igunga
Chacha ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya Timu ya ukaguzi wa mizani kutoka Wizara ya Kilimo iliyowasilishwa kwake na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Pembejeo za Kilimo Wizara ya Kilimo, Samson Poneja wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Ameeleza wametokea vishoka ambao wameweka chipu katika mizani hiyo na kusababisha wizi wa kila kwenye kilo 20 mkulima anaibiwa kilo 3.4 hivyo ikipimwa kilo 60 inaiba kilo 9.6, ikipima kilo 80 inaiba kilo 12.8 na ikipima kilo 100 inaiba kilo 15.
Amebainisha kwa mujibu watakwimu zilizowasilishwa kwake kilo 6.3 milioni zilikwishafanyiwa masoko, hivyo kwa wizi huu uliyoonekana hapa kuna kilo 998,967.7 zenye thamani ya sh. 599.380 milioni zimeibiwa na Viongozi wa AMCOS.
‘’Haya mambo ni lazima yakome, ni lazima mkome kuweka maji, mchanga na mawe hivyo Mhe. DC. ninaomba uniletee Polisi na TAKUKURU mko hapa, Mwenyekiti na Katibu Meneja wa AMCOS 32 wakapande kwenye gari la polisi,” ameagiza Chacha na kuongeza kuwa:
"Polisi na TAKUKURU nyinyi ni Watalamu hao watajitetea huko, hivyo atakaekutwa na hatia Kesho afikishwe mahakamani", amesema.
