Wagombea Ubunge majimbo ya Igunga na Manonga kupitia CCM wapeta katika uteuzi
MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amewateua wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge katika majimbo hayo.
Hamisi amefanya uteuzi huo leo Agosti 27 , 2025 katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mkoa wa Tabora.
"Nimekuteua Abubakar Alli Omari mgombea ubunge jimbo la Manonga na Kabeho Henry Charles mgombea ubunge jimbo la Igunga baada ya kukidhi vigezo," ameteua.
Aidha, amewatakia kila la kheri wagombea hao mchakato wa kampeni kuomba ridhaa kwa wananchi wawachague.
Ukuchukua fomu kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge lilianza Agosti 14 na leo Agosti 27, 2025 ndio mwisho huku wagombea wa CCM wakiteuliwa kugombea nafasi walizoomba.
Wagombea Ubunge majimbo ya Igunga na Manonga kupitia CCM wapeta katika uteuzi
Reviewed by Gude Media
on
August 27, 2025
Rating:
