Balozi Mulamula afanya mazumnguzo na Mjumbe Maalumu Katibu Mkuu wa UN Balozi Xia Huang
Na MWANDISHI WETU
Mjumbe Maalum wa Masuala ya Wanawake Amani na Usalama Barani Afrika, Balozi Liberata Mulamula, amekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Amani na Usalama wa Kanda ya Maziwa Makuu (UN Special Envoy on the Great Lakes Region), Balozi Xia Huang katika mazungumzo maalumu ya kubadilishana uzoefu wa kiutendaji.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Nairobi Kenya katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa UN, Balozi Xia Huang.
Balozi Mulamula alisema "Leo nimekutana na Miumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Amani na Usalama kwenye Kanda ya Maziwa Makuu( UN Special Envoy on the Great Lakes Region), Mhe. Balozi Xia Huang.
" Tumebadilishana mawazo kuhusu majukumu yetu na umuhimu wa kushirikiana kwa karibu hususan kwenye mchakato wa kuleta amani ya kudumu Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Xia Huang alimpongeza na kumshukuru Balozi Mulamula kwa kazi kubwa anayoifanya huku akimuahidi ushirikiano wa muda wote katika utekelezaji wa majukumu yake ya kudumisha amani na usalama.
