Dk. Nchimbi aitikisa Kahama aeleza sababu ya Dk. Samia kuchaguliwa tena
Mgombea Mwenza wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga.
Nchimbi akihutubia wananchi wa kahama amesema Dk. Samia anayo kila Sababu ya kupigiwa kura ya ndiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, amejipambanua katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali za wananchi na kufungua fursa kwa Watanzania.
Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama mjini, Benjamin Lukubha Ngayiwa na madiwani.
Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
