DKT. TULIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 27, 2023 Jijini Luanda nchini Angola.


Dkt. Tulia ameshinda Urais huo baada ya kupata kura 172 kati ya kura 303 zilizopigwa na anarithi mikoba ya Rais aliyemaliza muda wake, Duarte Pacheco kutoka Ureno.


Wagombea wengine walioshiriki Uchaguzi huo ni Catherine Hara kutoka Malawi kura 61, Adji Diarra kutoka Senego kura 51 na Marwa Hagi kutoka Somalia kura 11.