JESHI LA POLISI WAKAMATA WATUHUMIWA WA UTAPELI WA MTANDAONI
DAR ES SALAAM, POLICE KANDA MAALUMU
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalumu cha
kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao, wamewakamata wakazi wa Morogoro, Wilfred Werandumi na Abdulrahim Mwakibinga kwa tuhuma za kutumia majina ya viongozi serikali kutapeli wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa hao walijifanya wanaomba michango ya harusi, misiba na matibabu kwa viongozi mbalimbali wa serikali.
Muliro amesema baadhi ya viongozi ambao majina yao yametumika katika utapeli huo ni Waziri wa Ulinzi a Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Nchengerwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandsi Hamadi Masauni na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Daniel Chongolo.
Pia Muliro amesema wamewakamata wakazi wa Mbalizi mkoani Mbeya, Salum Kingu na Loveness Silonga kwa tuhuma za kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook, yenye jina la
KOPA FASTER TULIA TRUST FOUNDATION na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa watu mbalimbali kwa kudai kuwa wanatoa mikopo kwa masharti nafuu na haraka.
Amesema Polisi inaendelea na ufuatiliaji mkali wa tabia hizi na watuhumiwa wote watashughulikiwa vikali kwa mujibu wa sheria.
Wakati huo huo, Polisi kwa kushirikiana na kikosi hicho, wamewakamata mkazi wa Kawe, Claudian Makaranga (28) na
mkazi wa Kigamboni, raia wa China, Hongliang Yang (35) Mchina, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya
mawasiliano ya intanet nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.
Muliro amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia
mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.
Amesema vifaa vilivyoingizwa nchini imebaika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo
ya Dar es Salaam, kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Muliro amesema vifaa vilivyokamatwa ni Starline Dish 12, Starlink Router 12.
Aidha Muliro ametoa wito kwa wananchi wawe makini na matumizi ya vifaa vya
mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika.
Reviewed by Gude Media
on
March 22, 2024
Rating:
.jpeg)