KAMPENI YA ELIMU YA MLIPA KODI MLANGO KWA MLANGO YA TRA YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA MKOANI SHINYANGA
SHINYANGA, TRA
Maofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano, wamefunga kambi katika Mkoa wa Shinyanga kutoa elimu ya mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara wa mkoani humo mjini na vijijini.
Kampeni hiyo inaenda na ukusanyaji wa maoni na changamoto na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara hao kwa lengo la kuyafanyia kazi ili kuboresha zaidi na kurahisisha ulipaji kodi kwa hiyari.
Miongoni mwa changamoto zilizoripotiwa ni umbali wa upatikani wa huduma, ambapo wafanyabiashara wanapotaka huduma za TRA wanalazimika kusafiri kwa masafa marefu kufuata huduma hiyo, jambo linalowaongezea gharama wanazotumia katika usafari na muda mwingi
Aidha, baadhi ya wafanyabiashara wamefurahishwa na kampeni hiyo, ambayo imewasaidia kufamahu mambo mbali mbali ya kodi na kushauri iwe endelevu ili waendelee kujifunza zaidi.
Reviewed by Gude Media
on
March 22, 2024
Rating:





