MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah amejiandikisha katika Daftari la Wapiga kura huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kujiandikisha kupata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowakata.
Akizungumza baada ya kujiandikisha, Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga, alisema kazi kubwa imefanyika mkoani humo, kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kujiandikisha huku wakojitokeza Kwa wingi kila siku.
"Tangu zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura limeanza, kazi kubwa imefanyika, nilikuwa nikitembea maeneo mbalimbali kuwahamasisha wananchi wajiandikishe na leo nimekuja hapa nyumbani Pangani, nikaona na mimi nijiandikishe,"
Pis Abdallah alimpongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ikiwemo hamasa ya wananchi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura na kutekeleza miradi ya maendeleo, huku akiwashuku viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Tanga kwa kazi kubwa waliyoifanya kutoa elimu ya umuhimu wa kujiandikisha.