Na MWANDISHI WETU
Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Exaud Kigahe, ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, amesema wataendelea kukarabati barabara mbalimbali jimboni humo, kuchochea uchumi wa wananchi na Taifa kwa ukuaji uchumi.
Kigahe ameyasema hayo, wakati wa ziara jimboni humo, na kukagua miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa kwa kiwango cha lami.
Amesema Barabara inayotekelezwa kwa kiwango cha lami ni Mtili_Mkuta Ifwagi yenye urefu wa Kilometa 14 kiasi cha sh. bilioni 21 yenye uwezo wa kupitisha Tani za mzigo 30.
Ametaja zingine ni Barabara ya Usokami, Mapanda ni kipande cha Msitu Ihang'ana kutoka Kibengu kuelekea Igeleke na Mapanda.
"Barabara hii imetanuliwa kutokana na ufinyu wa awali.
Mara nyingi kulikuwa na ajali hasa katika Msitu(kwenye kona) huo kutokana na ufinyu.
Katika hatua nyingine, Mbunge Kigahe alichangia sh. Milioni 10 kwa ajili ya shughuli za maendeleo kama ujenzi wa Bwalo Shule ya Sekondari Mdabulo Kata ya Mdabulo.