LATRA- USAFIRI WA WAYA UTACHOCHEA UTALII MJINI

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini, (LATRA), imesema usafiri wa waya ni muhimu katika kurahisisha huduma hiyo, mijini hivyo ukianza utasaidia kufanikisha dhamira ya Rais Dk.Samia ya kuchochea utalii maeneo ya mjini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo katika kikao cha wadau wa usafirishaji Ardhini kujadili sheria na kanuni za usafirishaji Ardhini.

Amesema usafiri huo, wa Waya mijini, utasaidia kuchochea jitihada za Rais Dk.Samia za kukuza utalii wa miji, ambapo wanaendelea kujifunza namna bora ya uendeshaji kushirikiana na NEMC na Wakala wa Misitu.

"Hivyo kanuni hiyo itaangalia usalama wa kuwekeza katika miundombinu yake na usafirishaji wake kuhakikisha usafiri unakuwa salama," amesema.

Amesema LATRA wanajukumu la kuhakikisha kuwa usafirishaji unakuwa salama kupitia udhibiti wa sheria na kanuni ambapo wataendelea kuzisimamia vyema.