Liberata Mulamula - Kagera ya sasa imeamka kimaebdeleo, kuvutie uwekezaji na utalii



BALOZI, Mbunge Liberata Mulala amesema kuna kasi kubwa katika kuendeleza Mkoa wa Kagera kutokana na hamasa kubwa iliyopo ya ushirikishi kwani umejaaliwa neema na fursa nyingi za maendeleo.

Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo, wakati akizungumzia ushiriki wake katika tamasha la ‘Ijuka Omuka’ lililofanyika Kagera, lenye lengo la kuhamasisha wanakagera kukumbuka Mkoa wao na kuchochea maendeleo kupitia uwekezaji.

“Nimefurahi kushiriki katika tamasha hili la ‘Ijuka Omuka’ limetuhamasisha kuwa, wakuujenga Mkoa wa Kagera ni sisi wanakagera wenyewe sio mtu mwingine. Tamasha hili lilianza mwaka jana, ni zuri nimekuwa nikishiriki, kwa kweli limeendelea kutuhamsha.

“Tunamshukuru na kumpongeza Mkuu wa Mkoa, amekuwa sehemu ya kuleta hamasa zaidi katika tamasha hili kubwa, tumeshuhudia taratibu mbalimbali za kuhamasisha uwekezaji zikiendelea katika kipindi kizuri cha uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, chenye hamasa kubwa ya maendeleo hadi vijijini, kwakweli tunafurahi kwa hatua hii,”alisema