Na MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba,amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, amesikia kilio cha muda mrefu cha Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli na -wananchi wa jimbo hilo kuhusu changamoto ya barabara na kuahidi kuanza utekelezaji wa ujenzi.
Ameyasema hayo, wilayani Ilala, leo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara katika Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam.
Katimba amesema tayari Rais Dk. Samia, ametoa fedha kiasi cha zaidi ya sh. Milioni 475. Kujenga Barabara ya Bonyokwa-Zahanati kilometa 0.3 kwa kiwango cha lami katika Jimbo hilo.
“Pia Rais Dk.Samia, ametoa sh. milioni 902 kujenga Barabara ua Bonyokwa mwisho kilometa 0.5,” ameeleza Katimba.
Kuhusu Barabara ya Segerea Kusini, Maibu Waziri huyo, amesema itafanyiwa usanifu wa kina na itahusisha pia ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji.
“Mbunge ni kuhakikishie Rais Dk. Samia, amesikia kilio chako ndiyo maana alitoa fedha hizi zitakazo jenga barabara hizi,” alibsinisha Katimba.
Amebainisha pia barabara nyingi za jimbo la Segerea zimeingizwa katika Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP) awamu ya pili ambayo utekelezaji wake uko mbioni kuanza.
Naibu Waziri Katimba amesema katika utekelezaji wa mradi huo,Mkoa wa Dar es Salaam, jitihada zake pua zimeingeza bajeti ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA).
“Tumeona bajeti ya TARURA ngazi ya mkoa imeongozeka kutoka sh. bilioni 25 hadi zaidi ta sh.bilioni 50 kwa mwaka,” alisema Katimba.
Alieleza katika ngazi ya Wilaya bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka sh. bilioni 5 hadi bilioni 13 kwa mwaka.
Katimba aliwataka wakandarasi wanaopewa zabuni za ujenzi kutekeleza kwa mujibu wa mkataba na kwa wakati ili kufikia azma ya Rais Dk. Samia.
“ Pia wananchi wanataka kuona barabara zinakamilika, hivyo wakandarasi wahakikishe wanatekeleza kwa mujibu wa mkataba,”ameeleza
Awali Mbunge wa Segerea, Bonnah alimweleza Waziri huyo kuwa hali ya barabara katika jimbo hilo ni mbaya hasa wakati huu mvua inapoendelea kunyesha.
“Tunaomba wakandarasi mliowapangia kujenga barabara hizi waanze kazi. Miundo mbinu yetu ni mibovu. Mvua ikinyesha kidogo barabara zina jaa maji,” amesema Bonnah.