Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) kupitia huduma mpya ya Inbound Travel Insurance limemsafirisha mtu mmoja raia wa Kenya ambae alipatwa na changamoto za kiafya wakati akiwa visiwani Zanzibar.
Muda mfupi baada ya kupokea taarifa za kitabibu kutoka Hospitali ya Ampola Tasakhta kuhusiana na mgonjwa huyo, wafanyakazi wa Shirika la Bima la Zanzibar wakiwa na timu ya usafirishaji wa dharura kutoka Kampuni ya State Aviation waliweza kumsafirisha mgonjwa huyo na kumpelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.
Tukio la kumsafirisha mgonjwa huyo lilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja majira ya saa nne asubuhi ambapo gharama zote zimelipwa na bima ya Inbound Travel Insurance ambayo alikuwa nayo wakati alipopatwa na changamoto ya kiafya.