Mwandri amtaka mkaguzi wa pamba Wilaya ya Igunga kuzifungia AMCOS zitakazobainika kuchukua pamba chafu
IGUNGA TABORA
BALOZI wa Pamba Tanzania, Agrey Mwandri amemtaka Mkaguzi wa Pamba wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kuzifungia AMCOS ambazo zitabainika kuchukua pamba chafu.
Mwandri ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara yake katika vijiji vya Bulenya, Migongwa, Mwashiga, Itunduru, Mibuyumiwili, kagongwa na mwabalaturu kwa lengo la kutoa elimu ya usafi na ubora wa pamba kuinua kipato kwa wananchi.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Sauda Mtondoo amezielekeza AMCOS kukagua na kupokea pamba safi huku akiwataka kutochanganya pamba inayoonekana ipo daraja la pili.
Amewasisitiza kung'oa maotea hususan watakapopata fedha kuzitumia vema na kutenga za kuweka vibarua kwa lengo la kungoa maoteo jambo ambalo litawapa manufaa watakapokua na pamba safi.
