Wakulima wa zao la pamba watakiwa kufahamu thamani ya zao hilo
IGUNGA TABORA
WAKULIMA wa zao la Pamba nchini wametakiwa kufahamu thamani ya zao hilo haiishii kutengeneza nguo ispokua kupata mafuta ya pamba na mashudu yanayotakiwa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kulisha wanyama kupata maziwa mengi na nyama.
Akizungumza na kuonesha kivitendo namna ya kuvuna Pamba bora na safi kwa Wakulima wa zao hilo kutoka katika vijiji vya Mwagala, Ibole, Mwakwangu, Kalangale, Mwaomba na Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, Balozi wa Pamba nchini, Aggrey Mwanri amesema Wanunuzi wanaotoka katika nchi za China, India ikiwemo Marekani wanataka pamba safi.
Kwa mujibu wa Takiwimu za Benki ya Dunia, kiwanda cha kuchakata mbegu za Pamba kitakachojengwa Kata ya Mbutu wilayani Igunga kitakua na manufaa lukuki ikiwemo wananchi kupata ajira na Halmashauri kuongeza mapato.
Amefafanua kuwa kiwanda hicho kitaajiri wananchi 5000 wa Igunga ambapo kila mmoja anakadiriwa kuwa na watu 100 ambao wanamtegemea, hivyo ni vema waendelee kuzalisha pamba safi na bora kwa lengo la kujihakikishia kuipata fursa hiyo.
