JESHI LA MAGEREZA LIMEADHIMISHA MIAKA 64 KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA IGUNGA
IGUNGA - TABORA
MRAKIBU Mwandamizi wa Jeshi la Magereza wa Wilaya ya Igunga mkaoni Tabora, Kaganyero Kegori amewaongoza askari wa jeshi hilo kuchangia damu zaidi ya chupa 13 katika Hospitali ya wilaya.
Kegori amefanya zoezi hilo katika Hospitali ya wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Jeshi hilo kutimiza miaka 64 baada ya uhuru wa nchi hii.
‘’Sisi ni sehemu ya jamii tunachangia damu kwa lengo la kuendelea kuokoa baadhi ya wananchi ambao wanauhitaji wa Damu,” amesema.
Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Jesto Maguzu amelishukuru jeshi hilo kwa namna ambavyo wamejitoa kufanya usafi na kuchangia damu huku akitoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea kujitolea kwa sababu uhitaji upo.
