Kairuki achukua fomu za uteuzi ubunge Jimbo la Kibamba
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mgombea mteule wa Ubunge Jimbo la Kibamba, wilayani Ubungo, kupitia CCM, Angellah Kairuki, amechukua fomu ya uteuzi kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu.
Kairuki amekabidhiwa fomu hizo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jiimbo la Kibamba na Ubungo, Rose Mpeleta.
Baada ya kuchukua fomu, Kairuki amessema yupo tayari kuwatumikia wakazi wa Kibamba endapo watampa ridhaa yao.
Amesema atafanya kampeni za kistaarabu na kuheshimu demokrasia na mshikamano wa Kitaifa.
Kairuki achukua fomu za uteuzi ubunge Jimbo la Kibamba
Reviewed by Gude Media
on
August 25, 2025
Rating:
