Timoth achukua fomu za uteuzi ubunge Jimbo la Kawe
Na MWANDISHI WETU
Mgombea ubunge Jimbo la Kawe, Geofrey Timoth, amechukua fomu za uteuzi kugombea ubunge katika Jimbo la Kawe, wilayani Kinondoni.
Timoth amewashukuru wanachama na wapenzi wa CCM katika Kata zote za jimboni kwa kumsindikiza kuchukua fomu hizo, ambapo ameahidi kufanya kampeni za kistaarabu.
Pia amewakumbusha wananchi na wanaCCM, kushiriki katika uzinduzi wa kampeni za Chama kitaifa zinazotarajiwa kuzinduliwa August 28 mwaka huu, viwanja vya Tanganyika Perckas.
"Nimeona nichukue fulsa hii kuwakumbusha na nitaendelea kuwakumbisha mara kwa mara kwenda kushiriki uzinduzi huo kitaifa kwani ni neema kwetu kuletewa uzinduzi huo kwenye jimbo letu, ni vyema tujitokeze kwa wingi tukaujaze uwanja", alisema Timoth.
