ASANTE RAIS DK. SAMIA DMDP II NI FARAJA KWA WANANCHI WA TEMEKE - DOROTHY KILAVE

 

Na MWANDISHI WETU

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave, amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mradi wa Uendezaji wa Jiji la Dar Salaam, (DMDP II), ambao utakuwa msaada mkubwa kukarabati miundombinu ya Jimbo hilo ikiwemo barabara na mitaro.

Dorothy ameyasema hayo, leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji Saini ya mikataba ya zabuni nane kati ya serikali na mkandarasi, iliyofanyika vinwanja vya Mwembe Yanga wilayani humo.

Amesema imekuwa faraja kubwa kwa wananchi kuona mradi huo unaanza kutekelezwa kwani utaondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili ikiwemo suala la miundombinu.

Dorothy amesema wanamshukuru Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kwa kufanikisha suala hilo, huku akimpongeza Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mradi huo uliowagusa wananchi wa Temeke.

"Mh, kwa furaha niliyonayo sitaki kusema mengi nisije kulia, kwamaana mradi huu tuliusubiri na kuusemea sana na sasa umefika, tunakushukuru na kukupongeza,Waziri,  tuko tayari kusimamia kuhakikisha unafanyika vizuri na kuwa msaada kwa wananchi," amesema.