RAIS DK. SAMIA KUWEKA HISTORIA UTEKELEZAJI MRADI WA AWAMU YA PILI WA DMDP HALMASHAURI TANO DAR ES SALAAM

Na MWANDISHI WETU

HISTORIA imeandikwa katika Jiji la Dar es Salaam, baada ya  utiaji saini mikataba nane ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Halmashauri tano za mkoa huo, kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji (DMDP II) awamu ya pili, wenye  thamani ya zaidi ya sh.Trioni 1.18 sawa na Dola za Kimarekani  447.

Halmashauri zitakazo nufaika ni Tekeme, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo huku mradi huo ukiwa na jumla ya kilometa mraba za lami  250, mifereji yenye kilometa 90, stendi za mabasi tisa, masoko 18 na madambo matatu ya taka ngumu.

Akishuhudia utiaji saini katika hafla ya mradi huo, iliyofanyika Wilaya ya Temeke, viwanja vya Mwembe Yanga, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, alimshukuru Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kufanikisha mradi ulioweka historia kubwa na kubadilisha jiji hilo.

Amewaagiza viongozi wa Mkoa huo, Wizara na TANROADS kusimamia vyema mkadarasi kutekeleza kazi kwa weledi na kukamilisna kwa wakati kwani hawataongeza muda.

Pia, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, kuhakikisha acheleweshi  suala la  kuanzisha Jiji  la Dar es Salaam lifanyike kabla ya 2025, ikiwa ni maelekezo ya Rais Dk. Samia kuinua uchumi wa wananchi ambapo wanaendelea na mkakato wa utekelezaji mradi wa bonde la  mto msimbazi lenye hekta 57.

"Jambo hili linaonesha nia nje ya serikali ya Rais Dk.Samia  katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali barabara, masoko, vituo vya mabasi, miradi ya taka ngumu.