CHUO CHA BANDARI CHATOA KONGOLE KWA SERIKALI KWA UWEKEZAJI MADHUBUTI WA KUWEZESHA MAFUNZO BORA



Na MWANDISHI WETU

MKUU wa Chuo Cha Bandari Dk.Lufunyo Hussein ameishukuru serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Chuo hicho ikiwemo suala la uboreshaji wa miundombinu na vifaa vya mafunzo jambo ambalo limeendelea kuleta ufanisi wa mafunzo na kuzalisha wataalamu bora.

Pia, ameipongeza serikali ya Rais Dk.Samia kwa kuendelea kuongeza wataalamu wenye ubobevu ambapo kwasasa wana walimu saba wenye elimu ya Shahada ya Udhamivu PHD, ambapo kwa miaka ya minne nyuma walikuwa na Mwalimu Mmoja mwenye elimu hiyo.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema wanaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha ufanisi ikiwemo Taasisi binafsi ikiwa ni jitihada za serikali za kuimarisha Chuo na Bandari, kupata wataalamu.

"Tumekuwa na ushirikiano mzuri kwa sekta binafsi za hapa ndani na zingine za mataifa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora za mafunzo inayokidhi viwango vya kimataifa,"alisema.