BALOZI MULAMULA ASISITIZA KUJITAMBUA, KIJITUMA NA KUZINGATIA ELIMU KUFIKIA NAFASI ZA UONGOZI

Na MWANDISHI WETU

BALOZI Liberata Mulamula (Mbunge), amewasisitiza wasichana kujitambua na kujituma kama wana ndoto za kuwa viongozi, kwani hali hiyo itawasaidia kutimiza ndoto zao.

Balozi Mulamula ameyasema  jijini Dodoma alipozungumza na wanafunzi mbalimbali wa kike katika  siku ya maadhimisho ya mtoto wa kike dunia.

"Kama mna ndoto za kuwa viongozi, anzeni sasa kujituma na kuonyesha uwezo wenu.Vijana wengi wa sasa wanataka kubebwa, mjiamini na kuweka juhudi itawasaidia kufikia ndoto zenu," alisema.

Alisisitiza kuwa, ilikuwa kiongozi bora ni vyema wakazingatia maadili, uzalendo, kujituma na kushika elimu zaidi ambayo ni msingi mkubwa wa kufikia ndoto zao.