Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge Jimbo wa Jimbo la Mbeya Mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo Oktoba 20,2024 amejiandikisha kwenye Orodha ya wapiga Kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Dkt. Tulia amejiandikisha katika kituo cha Uzunguni A Kata ya Sisimba Mbeya Mjini na amewataka Wananchi ambao hawajajiandikisha kutumia Muda uliobaki kujiandikisha ili waweze kutumia haki yao ya Msingi ya kuwachagua Viongozi wanaowataka Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.