MWENYEKITI WA CCM TANGA-TUKO TAYARI KWA UCHAGUZI KUWAGALAGAZA WAPINZANI

Na MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, amesema wako tayari kwa uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwani wamejipanga vya kutosha kuwagalagaza wapinzani.

Pia, amewata wananchi wa Tanga kuendelea kujiandikisha katika daftari la kupiga kura, kupata fursa ya kuwachagua viongozi wanao wataka watakao waletea maendeleo.

Mwenyekiti Abdallah ameyasema hayo jijini Tanga, wakati akiendelea na hamasa ya kujiandikisha katika daftari la Kudumu la Wapiga kura.

Amesema Tanga hamasa nikubwa ya kujiandikisha, hivyo wanaimani kuwa itawawezesha kufanya vizuri katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupata viongozi wanaotokana na CCM.