Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo ya ramani kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, wakati bodi na menejimenti ya mamlaka hiyo ilipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma. |