TAASISI YA SINGASINGA YATOA MSAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA CHAMAZI NA MBAGALA















 

Jumuiya ya Singa Singa, imefanya maadhimisho kwa kumbukizi ya Mtume wao wa 10, Guru Gobind Singh, kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na vifaa vya kujifunzia wanafunzi, kwa vituo vya kulea yatima, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Vituo vilivyopata msaada huo ni Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Magengeni na Kituo Yatima Hiyari, kilichopo Mbagala Kizuani, wilayani humo. 

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Singa Singa ya Shri Guru Singh Sabha, Pirthipal Singh, amesema wakati huo mtume wao alipigania haki za binadamu na utawala, uliojulikana Mughal's.

Akizungumzia kuhusu mtume huyo, Singh, amesema wakati huo kulitokea vita ambapo waumini 40 walipigana vita hiyo na takribani wanajeshi milioni 1, pia mtume hakutorosha watoto wake wawili ambao walishiriki katika vita hadi walipoaga dunia (Shahidi).

Pia Singh amesema watoto wengine wawili wenye umri wa miaka saba na tisa, walishikiliwa na utawala wa wakati huo, waliwaadhibu kwa sheria ya wajengwe ukuta wakiwa hai.

Amesema ndipo kwa haya yote kama jamii wanapata mafundisho ya kujitolea na kusaidia jamii na upendo bila kujali itikadi ya dini.