Tigo yakabidhiwa tuzo ya Ookla

Ofisa Mkuu wa Teknolojia na Taarifa wa Tigo, Emmanuel Malya (kulia), akipokea tuzo ya mtandao wenye kasi zaidi nchini ya Ookla kutoka kwa Mkuu wa Tasisi ya Ookla Afrika Mashariki na Kati, Tristan Muhadeer,  jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Tigo Tanzania yakabidhiwa rasmi tuzo ya Mtandao Wenye Kasi zaidi Tanzania kwa mwaka wa 2023 iliyotolewa na taasisi ya  Kimataifa ya Ookla.


Ookla ni taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa huduma za intaneti duniani,ikiwemo speed/kasi ya intaneti na muda wa kupakua au kupakia maudhui mtandaoni. 


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Teknolojia Taarifa wa Tigo, Emmanuel Malya, alisema tuzo hiyo ni matunda ya uwekezeji unaoendelea kufanywa na Tigo Tanzania ili kuboresha miundombinu ya mtandao.


"Kama mnavyofahamu mwaka 2022 Tigo Tanzania ilianza kutekeleza mpango wa miaka mitano unaolenga kuwekeza kiasi cha shilingi za kitanzania zaidi ya Trilioni moja kwenye miundombinu ya mtandao wetu. 


"Uwekezaji huu pia, ni moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Axian Telecom Group, inayomiliki kampuni ya Tigo Tanzania," alisema.