TMDA YAKABIDHI MAGEREZA MWANZA DAWA ZA SH. MILIONI 56



Jeshi la Magereza Mkoa wa Mwanza, limeishukuru Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Tanzania (TMDA) kwa msaada wa dawa zenye  thamani ya sh. Milioni 56.

Akipokea msaada huo kutoka jwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza  ( SACP) Justin Kaziulaya, amesema dawa hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika magereza mkoani humo na kuishukuru TMDA kwa msaada huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, ameishukuru TMDA kwa maaada wa dawa hizo  kwa jeshi hilo muhimu.

Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki,Sophia Mziray, amesema mamlaka hiyo inatambua umuhimu wa jeshi hilo na kuona umuhimu wa kushirikiana hususan katika sekta ya afya.