Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida, Thomas Apson. |
Na HEMEDI MUNGA, Singida
Waandishi wa Habari nchini wamekumbushwa kuwaenzi viongozi waliotangulia mbele za haki ambao walikua na mchango mkubwa, kuhusu uhuru wa habari kila wanapokutana kuadhimisha siku hiyo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Thomas Apson, katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari kimkoa.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Kamishna wa Madini mkoa, zilizopo karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari na Wadau mbalimbali wa mkoa huo kuhusu uhuru huo, Apson amewakumbusha kuendelea kuthamini ikiwemo kuwaombea kheri viongozi waliohusika kuchagiza uhuru huo nchini.
Aidha, amesema licha ya kila awamu kuwa na mchango wake katika hilo, lakini Awamu ya Pili iliyoongozwa na Hatayati Ali Hassan Mwinyi ndiyo iliyofungua mlango wa mageuzi na kuleta demokrasia kwa mapana yake.
"Mzee wetu yule tunatakiwa tumuenzi sana kwa sababu anaalama kubwa katika nchi yetu," amesema.
Pia Apson ameendelea kumshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha uhuru wa kisiasa ambapo kwanamna moja au nyinge unakwenda sanjari na uhuru wa habari.
Ameeleza kuwa uhuru wa habari ni pamoja na kuwa huru kutoa habari, mawazo na maoni bila ya kiziwizi au kipingamizi kwa mujibu wa sheria.
"Tumpongeze Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katuweka katika mazingira mazuri ambapo kuna uhuru wa vyombo vya habari," amepongeza.
Ameweka wazi kuwa moja ya msaada unaowasaidia kuongoza vema ni kutokana na kupata habari.
"Nyinyi Waandishi wa Habari mnasaidia sana sisi viongozi kuongoza kwa sababu tunapata habari na kuzifanyia kazi kwa uharaka," amethibitisha.
Katika hatua nyingine, Apson ametoa wito kwa Wadau mbalimbali waendelee kushirikiana na Waandishi wa Habari kwa sababu wao ni jamii moja ambapo wanategemeana katika majukumu yao.
"Waandishi wa Habari hawakwepeki kwa sababu kazi za Wadau zitaonekana vipi na wapi", amesema.
Aidha, amewataka wanataaluma hao kuendelea kutengeneza mahusiano mazuri nakutotengenezeana mazingira ya kuumizana kwa kuwa wao ni wadau ambao ni lazima washirikiane.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa mkoa huo (SINGPRESS), Elisante Mumbiga, amesema wataendelea kusimamia maadili ya Waandishi waliowanachama na wasiowanachama mkoani hapa.
"Kwa kweli hapa tumekua wakali katika kusimamia maadili licha ya baadhi ya wadau kupuuzia mpaka pale wanapokabiliwa na matatizo ndio ukumbuka umuhimu wa chombo hichi," amesema.
Aidha, amemuhakikishia Mkuu huyo wa wilaya kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ya mkoa, Halmashauri za Wilaya na Wadau kueleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na mkoa huo.
Dunia uadhimisha Uhuru wa Habari kila ifikapo Mei 03, ambapo mwaka huu kidunia yalifanyika Akraa nchini Ghana na kitaifa ilikua jijini Dodoma.
&&&&&&&&&&&&&&
HABARI PICHA
01.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Thomas Apson akiwakumbusha Waandishi wa Habari mchango mkubwa wa viongozi kuhusu Uhuru wa Habari nchini, wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari kimkoa iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Kamishna wa Madini mkoa zilizopo karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. (Picha na Hemedi Munga)
02.