IGUNGA - TABORA
MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Sauda Mtondoo ameendelea kumshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) awamu ya tatu.
Sauda ametoa pongezi na shukrani hizo, wakati akizungumza na wanufaika wa mpango huo, ambao umewanufaisha wananchi 10, 323, katika Kijiji cha Njiapanda Kata ya Nkinga wilayani humo.
"Ndugu zangu wanufaika niwaombe tuendelee kufahamu serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja na sisi, hivyo nendeni mkaendelee kuzalisha kupitia ruzuku hii kwa lengo la kuendelea kujikwamua na umasikini," amesema.
Mpango wa Kunusuru Kaya masikini Awamu ya Tatu unatekelezwa katika vijiji vyote 119 ikiwemo eneo la Mamlaka ya Mji Mdogo wilayani humi na kutumia sh. bilioni 8.482.