Na Mwandishi Wetu
Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, inamshikilia Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Qiblaten Kawe, wilayani Kinondoni, kwa tuhuma za kumuua Mwalimu wake, Hassan Mohamed, baada ya kumshambulia kwa kisu shingoni na baadaye kupoteza maisha.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo Juni 20, mwaka huu saa 11.10 Alfajiri baada ya kumshambulia mwalimu wake aliyekuwa akiwahimiza wanafunzi wahudhurie ibada ya Alfajiri.
Muliro amesema majeruhi alifariki wakati akikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala, wilayani Kinondoni, ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo.
Amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.