Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simba Chawene akifungua Mkutano wa Watendaji atendaji Wakuu wa Wakala za Serikali, Dar es Salaam. |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema haridhishwi na baadhi ya wakala za serikali na kuomba watendaji wake kujitathimini.
Aidha amewataka Watendaji Wakuu wa wakala hizo kujitathimini kama wakala wanazoziongoza zimefikia mafanikio ama wameanza kufanya kazi kwa maazoea.
Waziri Simbachawene, amesema hayo leo, alipofungua Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali, Dar es Salaam, huku akisisitiza, watendaji kufuata madili, miongozo, mifumo na mabadiliko yanayofanyika katika kuleta tija.