SPIKA DK. TULIA AONGOZA KIKAO CHA MASPIKA WA CPA NCHINI CAMEROON


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza kikao wakati wa Mkutano wa 18 wa Maspika na Viongozi wa Bunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CSPOC) uliofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Yaounde Jijini Yaounde Nchini Cameroon.

Kikao hicho ambacho kinauadili athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani kimefanyika leo tarehe 19 Julai, 2023. Katika Mkutano huo Mhe. Dkt. Tulia ameambatana na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu pamoja na Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi.