DC MWENDA ASHIRIKI MAFUNZO YA MPANGO WA UONGOZI WA DUNIA NCHINI KOREA KUSINI

Na HEMEDI MUNGA 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda, yuko nchini Korea Kusini, kwa ziara ya kikazi kwa muda wa wiki mbili yenye lengo la kupata maarifa mbalimbali ikiwemo mafunzo ya uongozi.

Mwenda ameambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo, Msaidizi wa Waziri Mkuu katika masuala ya uchumi, Dk. Bariki Mwasaga na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Omar Ilyas.

Viongozi hao wapo nchini humo kushiriki  mafunzo ya Mpango wa Uongozi wa Dunia (Global Leadership Program) yanayotolewa na taasisi ya Korea Development Institute (KDI).

Aidha, mafunzo hayo yamehudhuriwa na viongozi 70 kutoka katika nchi 65 duniani.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda (wa pili kushoto), akizungumza na Balozi wa  Tanzania nchini Korea Kusini, Togolani Mavura, hivi karibuni. Kushoto ni Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuuu upande wa Uchumi, Dk. Bariki Mwasaga na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Omar Ilyas. (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya).