Katika jezi tatu ambazo zimezinduliwa hivi karibuni, jezi ya rangi ya bluu imekuwa adimu katika maduka yote haipatikani kutokana na kupendwa sana na mashabiki.
Baada ya kuzikosa katika maduka mbalimbali, mashabiki wameanza kuuziana kwa bei ya juu zaidi ya sh. 40,000 ambazo ni bei ya kawaida.
Mashabiki wameanza kuuziana jezi za rangi ya bluu kwa sh. 60,000 kutokana na kuwa ndio rangi inayopendwa na mashabiki wa timu hiyo.
Mzabuni wa jezi hizo, Sandaland The Only One', alisema mzigo upo wa kutosha, hadi kufikia siku ya Simba Day, kila mmoja atakuwa amepata jezi ambayo anataka.