WANAFUNZI IRAMBA KUPELEKWA DENMARK KUJIFUNZA

 

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda akieleza neema kwa wananfunzi takribani 25 wa wilaya hiyo kutembelea nchini  Denmark kwa lengo la kujenga uhusiano na kujifunza mambo mbalimbali nchini humo, leo katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri hiyo. (Picha na Hemedi Munga)







Na Hemedi Munga 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, ameleta neema kwa wanafunzi takribani 25 wa wilaya hiyo kutembelea nchini  Denmark kwa lengo la kujenga uhusiano na kujifunza mambo mbalimbali nchini humo.

Mwenda ametoa taarifa hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani robo ya nne kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, mkoani Singida.

Amesema madiwani hao wahakikishe walengwa wanapatikana kwa njia ya haki kwa lengo la kuondoa minong'ono kwa vijana watakaowawakilisha wenzao.

"Tumeomba kwenda nchini Denmark kufanya mahusiano ya kitaaluma, hivyo wiki iliyopita tumepokea mwaliko rasmi," amesema.

Amesisitiza kuwa suala hilo litakuwa endelevu huku wakitarajia kuanzisha uhusiano wa kiuongozi kati ya viongozi wa wilaya hiyo na viongozi wa nchi hiyo.

Mwenda amesema viongozi hao watapata nafasi ya kujifunza namna viongozi wa Denmark wanavyoongoza serikali zao za mitaa nawao  kujifunza viongozi wa wilaya hiyo wanavyoendesha serikali yao.

"Tunaoulazima wa kujifunza, ulazima wa  kuona namna wanavyoendesha serikali yao, kusimamia miradi yao na kuongoza watu wao," amesisitiza.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo Iramba, Innocent Msengi, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaletea fedha zote walizopanga katika bajeti ya Halmashauri hiyo.

Amesema haikuwahi tokea kwa wilaya hiyo kupanga bajeti halafu fedha zikaja zote ispokua katika kipindi hichi cha Rais Dk. Samia.

" Haijawahi tokea kutenga bajeti ya sh bilioni 32 zikaja zote ispokua katika kipindi cha Rais Dk. Samia kaleta zote, tunampongeza sana Rais wetu," amepongeza.

Anasema hakika Rais Dk. Samia anaupiga mwingi kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ira mba,Innocent Msengi, akimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha zote walizopanga katika bajeti ya Halmashauri hiyo, mkoani Singida, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo. ( Picha na Hemedi Munga).