MKAZI WA KIGAMBONI MBARONI KWA TUHUMA ZA KUWATUKANA VIONGOZI WA SERIKALI MTANDAONI

 













Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata na kumuhoji, mkazi wa Kigamboni, Selemani Gaya, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya viongozi wakuu wa Serikali  kwa kutumia mitandao wa kijamii. 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai  29 na wenzake, wamekuwa  wakitengeneza maudhui za mtandaoni (video) na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha  viongozi wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok.

Muliro amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani haraka izekanavyo. 

Muliro ametoa onyo kali kwa watu wanao toa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria. 

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Julai 31, 2023 limewakamata watuhumiwa saba  akiwemo Amani Kipolo mkazi wa Vingunguti kwa tuhuma za kumshambulia na kusababishia kifo Hadija Hamisi na kuwajeruhi watu wengine nane (8).

Watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wakiwa kwenye kundi waliwashambulia wananchi mtaani maeneo ya Vingunguti kwa lengo la kulipiza kisasi wakati wakitoka kuzimka mwenzao aliyefahamika kwa jina la Nurdin Bwino. 

Aidha, awali marehemu huyo Nurdin Bwino aliuwa kwa kushambuliwa na wananchi alipokuwa na wenzake sita wakiwa na visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia alipojaribu kuvunja nyumba moja usiku wa Julai 30, 2023.