KAYA 525 KUTOKA HIFADHI YA NGORONGORO KUTUA KIJIJI CHA MSOMERA

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi

Na Mwandishi Wetu 

Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi, amesema hadi kufikia Januari 12, 2024, kaya zilizojiandikisha kuhama kwa hiari kutoka  Hifadhi ya Ngorongoro ni 525,.

Amesema kati ya kaya hizo 525 kaya 126 zenye watu 812 na mifugo 2,581 tayari zimeshahama. 

Ameyasema hayo alipohitimisha ziara ya waandishi wa habari  kujionea hali halisi  ya  hifadhi hiyo na wananchi  walio hamis kwa hiyari katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni, Mkoani Tanga.

Matinyi amesema kaya zilizohama zimegawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza lenye kaya 74 lenye watu 520 na mifugo 1,599 limeenda Msomera na kundi la pili la kaya 52 lenye watu 292 na mifugo 982 wamechagua kwenda kwenye mikoa mbalimbali.

Amesema  kwa ujumla wake, mpaka sasa kaya 677 zimeshahama kwa hiari kutoka Ngorongoro zikiwa na watu 3,822 na mifugo 18,102. 

Amesema kesho kaya 72  zenye watu 515 litawasili Msomera kutoka   Ngorongoro.

Ameeleza ujenzi wa nyumba 1,000 uko katika hatua mbalimbali za ukamilikaji wake kijijini Msomera na wanchi watakabidhiwa bure, motisha ya sh. milioni 10 inayotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, magunia mawili ya mahindi na shamba.