MULIRO: UCHUNGUZI MAUAJI YA WATU WAWILI UNAENDEELEA


NA MWANDISHI WETU

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inachunguza tukio la mauaji ya watu wawili, Japhari Mwinyimvua (mlinzi)  na Richard Nonyo, baba mzazi wa mtu anayedaiwa ni mganga wa kienyeji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya  Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema tkio hilo limetokea Aprili 21, 2024, saa 3 asubuhi maeneo ya Kigogo fresh, Pugu, wilayani Ilala.

 Amesema mlinzi huyo alikutwa ameshambuliwa na baadae kupoteza maisha.

Muliro amesema hata hivyo katika mtiririko huo kundi la watu lilimshambulia baba mzazi wa mganga huyo na baadae akapoteza maisha wakimtuhumu mtoto wake kuhusika na kifo cha mlinzi huyo.

"Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wanachunguza  kwa kasi tukio hilo na wahusika wote wa tukio hili watakamatwa haraka iwezekanavyo  na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria", amesema.

Wakati huo huo, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imemkamata mkazi wa Masaki Furaha Dominick Jacobo na mkazi wa Mwenge TRA, Mustafa Kihenga kwa tuhuma za  uhalifu wa kimtandao kwa kusambaza picha chafu za video za watu zisizo na maadili kwa lengo la  kujipatia fedha kwa vitisho. 

Muliro amesema watuhumiwa hao  wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani  kujibu tuhuma zanazowakabili.