TAASISI YA TULIA TRUST YATOA BIMA AFYA KWA WATOTO 180 WENYE MAHITAJI MAALUMU MBEYA

MBEYA

Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge na Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt.Tulia Ackson imetoa msaada wa Bima za Afya kwa watoto 180 wenye mahitaji maalumu wanao lelewa katika kituo cha MBEYA CBR SIMAMA tawi la Uyole kata ya Itezi Jijini Mbeya. 

Kila mwaka taasisi ya Tulia Trust inatoa Bima za Afya kwa wakazi 6000 wa Jiji la Mbeya, hususan wale wanao ishi katika mazingira magumu na kutoa msaada wa matibabu, ikiwa ni mpango wa muendelezo wa kusaidia jamii katika sekta ya afya.