MWENGE WA UHURU WATEMBELEA MIRADI YA SH. BILIONI 17.3 ILALA

Na Mwandishi Wetu

MWENGE wa Uhuru umeendelea na mbio zake mkoani Dar es Salaam,, ambapo umeingia wilayani Ilala na kutembelea miradi sita yenye thamani ya sh. bilioni 17.3.

Akipokea mwenge  kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo,Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, alitaja miradi  hiyo kuwa ni Barabara  katika Mtaa  Ismail Upanga Mashariki yenye urefu wa kilomita0.65 wenye thamani ya sh. bilioni 1.6.

Pia miradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya  Liwiti iliyopo Mtaa wa Liwiti  unaogharimu sh.bilioni 3.5 na mradi ya wa ujenzi wa tanki la maji Kata ya Zingiziwa wenye thamani ya sh.milioni 11.2.

Mradi mwingine ni ujenzi wa Kituo cha  Afya Zingiziwa wenye thamani ya sh. milioni 636.5, shughuli za upandaji miti Zingiziwa yenye thamani ya sh.milioni 49.6,  miradi wa kikundi cha vijana  Kitunda kinacho endesha mradi wa utengenezaji vikoi na ushonaji wenye thamani ya sh. milioni 180.

Mpogolo alisema miradi hiyo  inatekelezwa kwa  fedha za mapato ya ndani ya halmashauri na serikali kuu.

KIongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu, alipongeza viongozi wa Wilaya ya Ilala na watendaji kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

"Katika barabara ya Isman mwenye umekagua  nyaraka za ujenzi ziko vizuri. Pia umekagua mradi wenyewe uko vizuri japo unakadoro ndogo ya mitaro.Tunataka ndani ya siku tano irekebishwe,"alisema Kaimu.

Katika mradi wa Sekondari ya Ghorofa Liwiti, Kiongozi huyo alitoa maelekezo ya kutafutwa matofali yenye ubora zaidi kumalizia sehemu ya juu.

Alisisitiza uwajibikaji, kupiga vita rushwa, matumizi ya dawa za kulevya,mapambano dhidi ya Maralia,Ukimwi, kuzingatia lishe bora na kutunza mazingira 

Mwenye wa uhuru ukianza mbio zake mkoani  Dar es Salaam, Mei 24 mwaka huu ukitokea Mkoa wa Pwani.

Tayari umetembelea Wilaya za Temek na Kigamboni, ambapo leo utaendelea na mbio zake Wilayani Ungo na kesho Kinomdoni kabla ya kuelekea Wilaya ya Mjini Magharibi Zanzibar.

Mkoa wa Dar es Salaam, jumla ya magoli radi 32 itapitia yenye thamani ya jumla ya sh. bilioni 23.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo, Dar es Salaam.