UCHUNGUZI WA KISAYANSI UMESAIDIA KUUNGANISHA WAHALIFU NA TUHUMA ZINAZOWAKABILI KIURAHISI.


Na. Jeshi la Polisi, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Nchini limeungana na wadau wengine dunia katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uchunguzi wa sayansi ya Jinai leo tarehe 20 Septemba, 2024 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kurasini.

Akizungumza kwa Niaba ya Kamishna Wa Polisi Uchunguzi wa Kisayansi, Mgeni rasmi katika halfa hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi, Mwamini Rwantale ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asili Jeshi la Polisi amesema hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la Polisi kuadhimisha maadhimisho hayo muhimu.

"Uchunguzi wa sayansi  ya Jinai umesaidia kuhakikisha  haki inatendeka kwa kuwa imesadia kubaini wahalifu  kirahisi na kuunganishwa na tuhuma zinazowakabili pasina shaka huku wasio na hatia kuachiwa huru", amesema.

Pia Rwantale amesema katika kusherekea siku hiyo kunaileta jamii pamoja kwani uchunguzi wa kisayansi ni wa kweli ambao husaidia kutenda haki.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, DCP. Dkt. Lazaro Mambosasa amesema uchunguzi hauruhusu kumuadhibu mtu ambaye hana hatia ambapo amesema uchunguzi wa kisayasi unaleta taswira njema kwa Jeshi la Polisi na Serikali katika kutenda haki.

Naye Ofisa kutoka Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa serikali, Fidelis Sekumba amesema uchunguzi wa kisayansi unatoa ushaidi wa uhakika zaidi na kunarahisisha maamuzi ya kisheria kwenye mihimili nayohusika kutoa haki.

Maadhimisho hayo hufayika kila mwaka 20 Septemba yakiunganisha wataalam wa uchunguzi wa kisayasi katika kutanzua uhalifu.