LATRA YAREJESHA HUDUMA ZA USAFIRI MABASI SITA YA KATARAMA


Na MWANDISHI WETU

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA),  imerejesha huduma za usafiri kwa mabasi sita ya kampuni ya Katarama Luxury kati ya mabasi 10 yaliyositishiwa leseni hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Salum Pazzy, amesema uamuzi huo umekuja baada ya uchunguzi wa awali uliofanyika na LATRA kushiriikiana na jeshi la polisi kubaini magari manne ya kampuni hiyo kuchezea mfumo wa VTS. 

"Baada ya kusitisha leseni ya kampuni hiyo, uchunguzi ulifanyika  na kubaini mabasi sita hayakuingilia mfumo wa VTS, ndiyo maana wameamua kuyarejesha kuendelea kutoa huduma," amesema.

Amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kwa mabasi manne yaliyobakia ikiwemo basi lenye usajili namba T 420 EBR ,T836 EBR , T835 EBR na T 485 DXP,  mabasi sita yaliyo ruhusiwa kutoa huduma ni yale yanayofanya safari zake DAR -Mwanza, na Dar Bukoba.