Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar wa Salaam, Albert Chalamila, amesema anatarajia kutangaza opereseheni kali katika shule za msingi na sekondari zinazotoza michango ambayo ni kinyume cha utaratibu.
Amesema ataagiza wakuu wa wilaya mkoani humo kupita katika shule zote kubaini zinazotoza michango wazazi na wanafunzi ambayo haijapitishwa katika ofisi zao na ofisi yake ya mkoa.
Ameeleza, hayo wakati alipo kuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule mpya ya mikondo miwili kupitia Mradi wa BOOST katika Shule ya Msingi Kunduchi, jana.
Pia alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.
Chalamila amesema, licha ya serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan , kuondoa ada katika shule bado baadhi ya shule zinatoza michango bila kuidhinishwa na ofisi yake, wakuu wa wilaya ama vikao husika .
Ameeleza jambo hilo la michango limesababisha malalamiko mengi kwa wazazi.
"Kazi anayofanya rais ni kubwa mno ya kuwekeza kwa watoto ambao ndiyo nguvu kazi ya sasa majengo haya yanajengwa , moja ya kitu ambacho wazazi wanakilalamikia ni baadhi ya shule kubwa na michango ya karaha,"amesema Chalamila.
Amebainisha wapo walimu wenye nia njema pia walimu wenye nia ovu ambao hutumia michango hiyo kujipatia fedha kinyume cha utaratibu hivyo kuleta karaha kwa wazazi.
"Na wanaichonganisha seri na wananchi.Hili litadhibitiwa kwa sababu kunapokuwa na shule zenye ubora kama huu lazima tujikite katika ubora wa elimu inayo tokea," alisema Chalamila .
Amepongeza Wilaya ya Kibindoni kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan miundombinu ya elimu, barabara, afya na biashara.
Katika ziara yake wilayani humo jana, Chalamila, alikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Kibindoni kilichopo Mtaa wa Ada Estate, kitakachojengwa kwa mfumo wa ghorofa kwa thamani ya sh. bilioni 1.91.
Amewataka wakandarasi kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya fedha.
Akikagua ujenzi wa Barabara ya Seko Toure ya kilomita 3.5 kwa thamani ya sh. bilioni 5.6 kiwancho cha lami unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Kinondoni katika eneo la Oysterbay, Chalamila alipongeza baada ya kuridhishwa na kitengo chake.
Miradi mwingi ni ujenzi wa Kituo cha Dala dala na maduka Mwenge ambao uko katika hatua ya mwisho kukamilika.
Akizungumza na wafanyabishara ndogondogo wa Mwenge, Chalamila alito wiki moja kwa wafanyabishara hao kurudi katika soko maalumu lililopo katika makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Samnujoma na Cocacola.
" Wafanyabishara walioondoka katika soko hilo maalumu waatoke wenyewe mtaani na kurejea.Siyo nia ya serikali kutumia nguvu kwa sababu kuna madhara", amesema.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Sa'ad Mtambue, alisema wilaya yake hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha inatumia kwa usahihi fedha zinazotolewa na Rais Dk. Aamua na mapato ya ndani ya halmashauri.
Mtambule amebainisha, Rais Dk. Aamua alitoa kiasi cha sh.ilmilioni 500 kujenga Kiituo cha Afya Kibindoni,ambapo kiasi cha sh. milioni 200 zilitumika kujenga maabara na zingine zitatumika kujenga jengo jipya la ghorofa moja katika kituo hicho.
Mtambule amesema ipo miradi mingi inayotekelezwa wilayani humo ambayo inaenda vizuri ukiwemo ujenzi wa shule za ghorofa, barabara,uwanja wapira na maeneo ya biashara.