Na MWANDISHI WETU
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, huku akisema ulinzi na usalama umeimarishwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika salama.
Mpogolo, amepiga kura katika Kituo Namba moja, Mtaa wa Karume, Jijini Dar es Salaam, ambapo alisema wilaya hiyo ina jumla ya vituo zaidi ya 2496 katika mitaa 159 .
“Utulivu umeimarika, hali ya vifaa vya kupigia na usalama viko iko vizuri. Wananchi wameitikia wito wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Idadi ya watu waliojitokeza ni kubwa,” amesema.
Mpogolo amesema hali ya usalama imeamarishwa katika kipindi chote cha uchaguzi.
“Wanaotaka kufanya vurugu waache kupanga mikakakati hiyo kwa sababu jeshi la polisi limejiandaa kikamilifu.”ameeleza.
Aidha amewataka wananchi wanapomaliza kupiga kura kuondoka katika vituo hivyo kuendelea na majukumu mengine ya kulijenga taifa.