Kanyasu - Tutashinda kwa asilimia 100 uchaguzi serikali za mitaa

  


Na MWANDISHI WETU

Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu amesema kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) jimboni humo, watashinda kwa asilimia 100 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza na gazeti jimboni humo, kuhusu kampeni zinazoendelea jimboni humo, amesema zinaenda vizuri ambapo wanaendelea kuwanadi wagombea kila kata wanaotokana na CCM.

“Kampeni zinaendelea kwa kasi kubwa, hatuna shaka na uchaguzi huo, tumejipanga vizuri kwani hata ilani ya uchaguzi ndani ya Geita Mjini, imetekelezwa kwa asilimia 95, kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, hali ambayo imeweka imani kubwa kwao juu ya CCM na viongozi wake”amesema.

Kanyasu amesema kupitia mikutano hiyo wanazungumza sera na mafanikio yaliyotekelezwa na Rais Dk. Samia, viongozi mbalimbali kupitia fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.